Tuesday, August 2, 2016

Na Baraka Mbolembole

Miaka nane iliyopita kulichezwa mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika kati ya Simba na BDF X1 ya Botswana katika uwanja wa Uhuru,jijini Dar es Salaam,lilikuwa ni pambano la kwanza kabla ya wiki mbili baadaye Simba kusafiri hadi jijini,Gaborone.
Simba ilishinda kwa ushindi ‘finyu’ nyumbni kwa bao lililofungwa na Athuman Machuppa.

Kikubwa kilichonifanya nikumbuke mechi hiyo ni uwezo wa Machuppa na aina ya kipaji alichokuwa nacho cha kufunga magoli tena yale ya kuvutia.Kwa yule ambaye hakubahatika kuliona goli alilofunga Machuppa dhidi ya ‘watswana’ hao mwaka 2003,basi lilikuwa zaidi ya lile alilofunga,Wayne Rooney dhidi ya Manchester City wikend iliyopita.
Machuppa ‘smilling killer’ kama alivyokuwa akifahamika kwa wapenzi wa Simba alikuwa na uwezo mkubwa wa kufosi magoli kwa stahili ya mkali wa zamani wa ‘nyavu’ Duniani,Ronaldo de Lima,alikuwa mjanja na msumbufu kwa mabeki kama winga wa zamani wa Ureno,Sergio Concecao,pia kuna wakati alikuwa akionekana mshambuliaji mwenye nguvu kama nyota wa zamani wa Ujerumani,Carsten Jancker,zaidi alikuwa mviziaji kama ‘mfalme wa eneo la mita 18’ Phillipo Inzaghi.
Kitu kimoja ambacho naona tulikimiss kutoka kwa Machuppa ni kumnyima nafasi ya kuonesha na kulisadia taifa kutokana na kipaji chake.Kwa mchezaji mwenye kipaji na uwezo mkubwa wa kufunga mabao kama Machuppa ni aibu kumpa nafasi ya kuliwakilisha taifa kwa mechi zisizo zidi 15 katika maisha yake ya soka!!
Pamoja na kunyimwa nafasi bado Machuppa aliweza kufunga zaidi ya magoli saba katika mechi zote alizoichezea Stars.Kwa ufupi hakuna mshambuliaji bora na mfungaji katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kama Machuppa.
SAMATTA ANAWEZA KUWA KAMA MACHUPPA
Achana na mabao mawili aliyoifungia Simba dhidi ya Wacomorro,Elan,jumapili iliyopita au yale aliyoifunga timu yake’ iliyomlea’ African Lyon.Mbwana Samatta anaweza kuwa jibu la matatizo yote ya ushambuliaji nchini kwa sasa.
Ni kijana mdogo mwenye rekodi ya kuvutia katika ufungaji wa mabao.Ana wastani wa kufunga bao moja katika michezo miwili hadi mitatu anayocheza.
Samatta ana vitu vingi kama alivyokuwa Machuppa miaka ya nyuma,lakini yeye ana kitu cha ziada zaidi ya Machuppa,nacho ni uwezo wa kupiga mashuti yenye ‘uzito’ kama ya kina Patric Mboma ama mshambuliaji wa zamani wa Mexico,Juan Pablo Angel.Kama kinda hili litaachwa na kuwa huru kukua kimchezo ni wazi litakuwa ‘tishio’ kwa wapinzani wake wengi uwanjani.
Nchini Zimbabwe tayari wanaye chipukizi ‘hatari’ katika kufumania nyavu,Knowledge Musona ambaye wanamuona kama Peter Ndlovu mpya….nasi tunaye Samatta ambaye anaweza kuwa mfungaji mahiri zaidi ya kina,Machuppa na Sunday Manara.
Makala hii imeandikwa na Baraka Mbolembole.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video