Saturday, August 6, 2016

Jose Mourinho amesema kwamba Cristiano Ronaldo hakuwa na msaada wowote kwenye mchezo wa fainali wa Euro ambapo Ureno waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Ronaldo alilazimika kutoka nje katika kipindi cha kwanza baada ya kuumizwa na Dimitri Payet lakini haikuzuia timu hiyo kuibuka na ushindi na kutwaa ubingwa.

Mchezaji wa zamani wa Ureno na Benfica Antonio Simoes, alimkosoa Ronaldo kwa mbinu zake, na Mourinho amekubaliana naye kwamba, mchezaji huyo hakuwa na msaada wowte bali tu alizidiwa na hisia.

"Mchango wake ndani ya dakika za mwisho za mchezo wa fainali haukuwa chochote," Mouriho alikiambia kituo cha runinga cha Sport TV. "Kulikuwa na wachezaji 11 uwanjani ambao walikuwa wakitekeleza majukumu yao, na mtu pekee aliyekuwa akiwaongoza ni kocha tu basi."

"Kikubwa nilichokiona kwake ni kuzidiwa na hisia tu, kwa mtu yeyote ambaye aliiangalia timu vizuri, isingechukua muda mrefu kwako kufanya kile walichodhamiria.

"Alishindwa kudhibiti hisia zake, japokuwa sio kitu kibaya. Nadhani wachezaji 11 ambao walikuwa uwanjani kwa wakati huo, walikuwa na dhamira moja tu ya kutaka ushindi, na walikuwa wameonesha dhamira hiyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video