Tuesday, August 16, 2016

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Yanga Mzee Ibrahim Akilimali leo ameomba radhi kufuatia kauli yake ya kwamba wanachama wa klabu hiyo na Manji walikurupuka kutoa maamuzi juu ya kuikodisha timu hiyo.
Mzee Akilimali aliongea hayo wakati akihojiwa na radio E-fm ili kufafanua kauli yake hiyo, ambayo imesababisha hali ya sintofahamu klabuni hapo baada ya taarifa za kujiuzulu kwa Manji katika wadhifa wake wa uenyekiti.
Mzee Akilimali amesema: " Sijamtusi mwenyekiti wangu kwa kusema amekurupuka . Neno hilo ni la kawaida wala sikuwa na dhamira ya kumtusi mwenyekiti wangu , nawaomba radhi wana yanga kwa kauli zangu . 
"Usiku sijalala nilikosa raha mara baada ya kusikia Manji kajiuzulu. . Mie naomba tuwe na umoja tatizo letu na mwenyekiti ni kushindwa kutuita wazee kwenye mpango wake wa kuichukua timu."
"Sisi tunampenda na kumuhitaji sana Yusufu lakini tunahitaji aendeleze mfumo wa zamani alioanza nao wa kujali na kuthamini wazee ili nasi tujisikie vizuri na klabu yetu."
"Nasisitiza sina chuki na Manji maana kwa mdomo wangu huu nimeshiriki sana kumuweka madarakani mpaka pale umma wa watanzania wakasema tumevunja katiba . Ninachotaka alitambue baraza la wazee na sisi tukae nae tuzungumze mstakabali wa klabu yetu"

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video