Baada ya mchezo jana kati ya Simba na Ndanda ambapo Simba walipata ushindi mnono wa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kumekuwa na minong'ono mingi kuhusu mshambuliaji Ibrahim Ajib kucheza ilhal alikuwa na adhabu ya kadi kupewa kadi nyekundu msimu uliopita.
Msimu uliopita kwenye mchezo dhidi ya Mwadui iliofanyika Uwanja wa Taifa, Ibrahim Ajib alipewa kadi nyekundi ya moja kwa moja (straight red card ) na alipaswa kukaa nje kwa mechi tatu.
Ikumbukwe baada ya hapo Simba walicheza michezo mitatu ambayo yote Ajibu hakucheza. Michezo hiyo ni dhidi ya Majimaji uliofanyika mjini Songea, dhidi Mtibwa Sugar mjini Morogoro na wa mwisho dhidi ya JKT Ruvu (Uwanja wa Taifa).
Katika michezo yote hiyo, Ajib hakucheza kwani alikuwa yupo Afrika Kusini kwaajili ya kufanya majaribio.
Hivyo basi, adhabu yake alikwishaitumikia na kumaliza msimu uliopita na alikuwa huru kucheza mchezo wa jana.
Uthibitisho huu hapa.
0 comments:
Post a Comment