Thursday, August 25, 2016

Thabani Scara Kamusoko kiungo mkabaji na wakati mwingine mchezeshaji ni moja ya wachezaji mahiri na wenye nidhamu kubwa katika klabu ya Yanga.
Uwepo wake kwa kushirikiana na wachezaji wengine ulichangia kuipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Azam Sports Federation Cup pamoja kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, licha kushindwa kufuzu kwenda nusu fainali baada ya kumaliza nafasi ya mwisho kwenye kundi lao.
Leo mama yake ametimiza umri wake wa miaka kadhaa ya kuzaliwa na kuamua kumwandikia ujumbe mzuri wa kumtakia heri ya siku hii maalum kwake.
Kamuso, ambaye pia amekuwa na juhudi kubwa za kujua lugha ya Kiswahili ukilinganisha na wachezaji wengine wa kigeni amemuandikia mama yake ujumbe huo kwa kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Kamusoko ameandika: "Happy birthday mama yangu.....mungu akuongezee maisha marefu...i wish i was there to celebrate with you....love you mama and i mis you."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video