
Leicester City ndio mabingwa wa EPL msimu uliopita. Baada ya kuchukua ubingwa, mwenyekiti wa hiyo Vichai Srivaddhanaprabha aliahidi kununua gari kwa kila mchezaji wa timu hiyo kama zawadi kutokana na mafanikio yao ya kuipa ubingwa timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu ianzishwe. Jana wakati wanaenda mazoezini kwaajili ya kujiandaa na mchezo wa leo wa Ngao ya jamii dhidi ya Manchester United, wachezaji wengi walionekana na ndinga zao mpya aina ya BMW zenye thamani ya paundi 105,000 walizopewa na baada ya bosi wao kutimiza ahadi yake licha ya baddgi yao kutumia magari yao waliyonunua wenyewe.

Jamie Vardy alienda na gari lake badala ya lile la BMW ambalo walinunuliwa wachezaji wote

Beki Christian Fuchs aliendesha BMW la zawadi

Shinji Okazaki aliendesha gari lake la kila siku badala ya BMW

Riyad Mahrez alikuja na BMW 

BMW zenye thamani ya paundi 105,000 zikiwa zimepaki maskani ya Leicester kwenye uwanja wa King Power

0 comments:
Post a Comment