Friday, August 12, 2016

"Hatuwezi kushindana au kwashinda washindani wetu ambao wana pesa nyingi kuliko sisi. Tunapaswa kuwa makiini sana, kufanya machaguo sahihi."Hayo nia aina ya maneno ambayo kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakisikia kutoka kwa kocha na viongozi wao juu ya wapinzani wao. Ni Arsenal wenyewe kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wao Ivan Gazidis waliwaaminisha washabiki wa wapenzi wao kwamba, klabu ina akiba ya kiasi cha paundi mil 200 kwaajili ya usajili, hivyo wana uwezo wa kuleta mchezaji yeyote.

Bila kupepesa macho ni ukweli kwamba, Arsene Wenger ndiyo meneja bora tangu Herbert Chapman na ataacha historia kubwa pale atakapoondoka. Miaka ishirini ya kushiriki Ligi ya Mabingwa mfululizo yanabaki kuwa mafanikio makubwa kwake na klabu, makombe matatu ya Ligi ya England na sita ya FA bila kusahau kumaliza msimu wa ligi bila kupoteza mchezo ni jambo la kujivunia sana.

Hata hivyo, licha ya mambo yote hayo niliyotaja hapo juu ambayo ni ya kujivunia kwa klabu hiyo, Arsenal hawajatwaa taji la Ligi ya England kwa miaka 12 sasa, hawajavuka hatua ya 16 bora kwenye Uefa kwa miaka sita mfululizo na kuwa klabu pekee kwenye ligi kubwa tano Ulaya kutosajili mchezaji wa ndani kwenye dirisha usajili lililopita licha ya kuwa na uhitaji wa wachezaji

Mwanzoni mwa dirisha hili alianza kuwahadaa washabiki na wapenzi wa Arsenal. Pengine alikuwa kocha wa kwanza miongoni mwa makocha wa vilabu vikubwa barani Ulaya kuanza kusajili baada ya kumsajili kiungo Granit Xhaka kutoka Borussia Monchengladbach kwa ada ya paundi mil 35, kabla ya kumuongeza kinda wa Kijapan Takuma Asano, beki Rob Holding (20) na kinda wa Kinigeria  Kelechi Nwakali (18). Na kwa namna inavyoonekana ni wachezaji Xhaka na Holding pekee ndio watakaokuwa kwenye kikosi cha kwanza msimu huu, huku Asano and Nwakali wakisubiri vibali vyao kwaajili ya kutolewa kwa mkopo kwa ili kupata uzoefu zaidi.

"Inabidi tufuate gharama zinazolipwa na watu wengine," hivi karibuni Wenger alisema. "Bei zimekuwa juu sana kwasababu upatikanaji wa pesa uko juu sana. Na ndiyo maana unaona sasa tumevuka mpaka paundi mil 100 kwa usajili wa mchezaji mmoja tu.

"Tunataka kutumia pesa tulizonazo," aliongeza. "Lakini tunaheshimu pia pesa tulizonazo, ni vigumu sana kupata wachezaji wenye ubora halisi kwenye soko la sasa. Licha ya uwepo wa pesa nyingi sana hapa England lakini bado utaona watu wanafanya usajili taratibu sana.

Hayo ndiyo maneno ya Arsene Wenger ambayo kila siku amekuwa akiyasema. Arsenal wanahitaji nini hasa? Wanahitaji beki wa kati mwenye uzoefu wa kutosha kusaidiana na Per Mertesacker, Laurent Koscielny pamoja na Gabriel Paulista. Wanahitaji mshambuliaji mwingine wa kusaidiana na Olivier Giroud. Giroud tayari ameshidndwa kuonesh kila ambacho wenzake kama Thierry Henry na Robin van Persie walionesha katika nyakati zao. 

Ikumbukwe kwamba nyuma ya Giroud kuna fundi wa pasi Mesut Ozil ambaye msimu uliopita aliweka rekodi ya kutengeneza nafasi nyingi ikiwa ni pamoja na pasi za magoli. Sasa ili Ozil azidi kufanya kile wanachotarajia watu wengi, inahitajika straika mwingine wa kumpa changamoto Olivier Giroud na kutoa upinzani mkubwa kwa timu nyingine.

Kwa sasa Per Mertesacker and Gabriel Paulista watakuwa nje kutokana na kusumbuliwa na majeraha. Hii sasa imemlaziku Wenger kutoka kwenda kutafuta mbadala ambaye atazidi pengo hilo, na taarifa zilizopo zinadai kwamba Shkodran Mustafi anatajwa kumalizana na klabu hiyo hivi karibuni. Huyu walau atakuwa msaada mkubwa kutokana na ubora na uwezo wake wa kusoma mchezo, kitu ambacho Arsenal inahitaji kwa kiasi kikubwa kwa sasa.

Lakini wasiwasi unabaki kwamba, Je, Wenger ataleta mshambuliaji? Kushindikana kwa uhamisho wa Jamie Vardy na kuamua kubaki Leicester na kukataliwa kwa ofa yao ya kwanza ya paundi mil 29 na Lyon juu ya mshambuliaji Alexandre Lacazette ni mifano ya hai ya changamoto anayokumbana nayo Arsene Wenger kwenye nafasi ya ushambuliaji.

Siku 16, michezo mitano, nchi nne, magoli 17 ya kufunga na matano y kufungwa. Arsenal wamemaliza kwa namna hiyo msimu wao wa pre-season kufuatia safari zao kwenye nchi za Ufaransa, Marekani, Norway na Sweden. Walihitimisha mechi yao ya mwisho kwa ushindi mujarab wa magoli 3-2 dhidi ya Manchester City. Wameonekana kuimarika kwa kadri walivyozidi kucheza mechi zao za kirafiki.

Chuba Akpom ameonesha kuimarika baada ya kufunga kwenye michezo minne mfululizo. Ilielezwa kwamba angeweza kuanzishwa kwenye mchezo dhidi ya Liverpool lakini kiwango kizuri cha Walcott kwenye mechi mbili dhidi ya Viking FK na Manchester City kunaweza kusababisha aanze badala ya Akpom. Hata hivyo kwa jinsi hali ilivyo bado anahitajika straika mwingine mwenye 'killer instincts', Akpom bado hana uzoefu wa kutosha.

Ujio wa makocha kama Pep Guardiola, Jose Mourinho na Antonio Conte, jumlisha usajili wa wachezaji kama Zlatan Ibrahimovic, Paul Pogba, Ilkay Gundogan na N'Golo Kante, Arsenal watakuwa na kibarua kigumu sana msimu huu kwenye mbio za kuwania taji la EPL. Kwenye mchezo dhidi ya Liverpool watakuwa na wasiwasi mkubwa pale safu yao ya ulinzi itakapokuwa chini ya makinda wasio na uzoefu Rob Holding and Calum Chambers, huku mapema kabisa wakianza kuandamwa na mkosi wa majeruhi.

Kuna wasiwasi wa utimamu wa Santi Cazorla ambaye ametoka kuuguza majeraha yake ya goti bila kusahau spana mkononi Jack Wilshere ambaue pamoja na kutocheza kwa muda mrefu, majeraha yamekuwa sehemu ya maisha yake na sasa anasumbuliwa na maumivu ya goti.

Msimu huu ambao unaonekana kuwa na ushindani mkubwa zaidi kuwahi kutokea baada ya kipindi kirefu, unaweza kushuhudia Arsenal wakiangukia pabaya zaidi kama hawataenda na upepo unavyotaka. Bado kuna muda mwingi tu wa usajili, na kama Arsene Wenger akiendelea kubania pesa za usajili ama hakika anaweza kuandika historia mpya, huku akiwa anaelekea ukingoni mwa mkataba wake.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video