Tuesday, August 2, 2016

KIUNGO wa zamani wa Yanga SC, Salum Telela amewashukuru mashabiki wake aliowaacha katika timu hiyo na kusema kuwa sababu za kimasomo ndizo zimemfanya kuichagua timu ya Ndanda SC ya Mtwara na kuzitosa ‘ofa nono’ kutoka kwa baadhi ya timu nyingine ambazo zilihitaji huduma yake mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake na klabu ya Yanga, Juni mwaka huu.
“Walikuwa wema (mashabiki wa Yanga) sana kwangu kwa kipindi chote nilipokuwa mchezaji wa timu hiyo. Ni jambo jema sana kwangu kwa mapenzi waliyonionesha. Nawashukuru kwa hilo. Mpira ukiwa ndiyo kazi yangu bado nina ndoto za kurejea hapo siku moja ikiwa yatakuwepo makubaliano,” Telela ambaye anachukua masomo ya uhasibu ngazi ya Diploma katika Chuo cha Stella Maris Mtwara University College alinukuliwa na Shaffihdauda.com.
“Nimeichagua Ndanda kwa sababu nitakuwa kimasomo huku. Kwa sasa nipo Chuo Mtwara lakini timu imeshaanza mazoezi huko Dar es Salaam,” anasema Telela.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video