Mataifa mbalimbali yanaendelea kuzoa Medali katika mashindano ya Olimpiki ya Rio 2016 yanayoendelea Mjini Rio de Janeiro nchini Brazil.
Kama kawaida, Marekani mpaka sasa inaongoza kwa kuchukua Jumla ya medali 38 ambazo ni 16 za Dhahabu, 12 za fedha na 10 za Shaba.
China inashika nafasi ya pili kwa kutunukiwa jumla ya medali 30 zinazotokana na medali 11 za dhahabu, 8 za fedha na 11 za Shaba.
Nafasi ya tatu inashikwa na Japan ambao wamepata medali 7 za Dhahabu, 2 za Fedha na 13 za Shaba na Jumla wamejikusanyia medaili 22.
Hapa chini nimekuwekea 10 bora ya Mataifa yanayoongoza kutwaa Medali mpaka sasa.
0 comments:
Post a Comment