TAARIFA KWA UMMA.
klabu ya Simba kwa masikitiko makubwa imepokea taarifa ya msiba wa baba mzazi wa mchezaji wa kimataifa wa Yanga Deo Munishi,Mzee Bonaventure Ludovic Munishi kilichotokea juzi hapa jijini
Msiba huo ni pigo kubwa kwa golikipa huyo,familia yake.klabu yake na wapenzi wa mpira kote nchini hususan wanachama na wapenzi wa Yanga.
Klabu leo itawakilishwa na Makamu wake wa Rais Geoffrey Nyange Kaburu katika kuuga mwili wa marehemu Munishi._nyumbani kwake Temeke Mikoroshini saa tano asubuhi hii.kabla ya kusafirishwa kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi.
Mwenyezimungu awape moyo wa subira wafiwa na amrehemu marehemu
Ameen
Imetolewa na
HAJI S.MANARA
MKUU WA HABARI
SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA
0 comments:
Post a Comment