Luis Suarez amepiga hat-trick kwenye mechi ya ufunguzi wa La Liga wakati Barcelona ikiiangamiza Real Betis.
Arda Turan alianza kufungua mvua ya magoli kwa kuifungia Barca kwa shuti la karibu kabla ya Ruben Castro kusawazisha kwa mpira wa adhabu ndogo.
MessI akaongeza bao jingine alilofunga akiwa takriban mita 22 kutoka goli kisha Suarez akatupia kambani akiwa nje kidogo ya box.
Suarez akafunga goli la nne, hakuishia hapo, akaifunga bao lake la tatu kwa mpira wa adhabu ndogo baada ya Messi kufanyiwa madhambi kabla ya Castro kuifungia Baetis bao la pili dakika za lala salama.
Raia huyo wa Uruguay aliyeibuka mfungaji bora wa La Liga msimu uliopita akiwa ametupia wavuni magoli 40, ameifungia Barcelona magoli 17 katika mechi sita za mwisho.
Baada ya mchezo, Barcelona ilithibisha kuanza makubaliano na Manchester City kwa ajili ya usajili wa Claudio Bravo, golikipa huyo mwenye miaka 33 alianza kwenye mchezo dhidi ya Betis.
Suarez aliifungia Barca magoli muhimu na kuisaidia kushinda taji la La Liga msimu uliopita, akifunga magoli 14 kwenye mechi zao tano za ligi zote Barcelona ikishinda ikiwemo hat-trick kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Granada siku ya mwisho ya mechi ya La Liga.
Real Madrid wangeshinda taji la La Liga endapo Barca ingedondosha pointi kwenye mechi hizo.
Jumapili, Real Madrid iatakuwa ugenini kukabiliana na Real Socidad wakati Atletico Madrid wao watakuwa numbani kuwakaribisha Alaves.
Magoli aliyofunga Suarez katika mechi 6 zilizopita
4 v Deportivo La Coruna (8-0)
4 v Sporting Gijon (6-0)
1 v Real Betis (2-0)
2 v Espanyol (5-0)
3 v Granada (3-0)
3 v Real Betis (6-2
0 comments:
Post a Comment