Sunday, August 7, 2016

TUMUELEWE MANJI TUNUFAIKE
Kwanza napenda tuelewane kitu kimoja kikubwa sana hapa, katika mfumo wa sasa wa umiliki na uendeshaji wa klabu kubwa za yanga na simba KAMWE hazitaweza kuendelea bila ya kubadilisha mifumo hii, mana ilikuwepo tangu enzii zile za TANU na ASP.
Ilikuwa ni mifumo ya mpira wa kufurahisha na sio mifumo ya mpira wa biashara kama sasa hivi. Hivyo jambo la kwanza ambalo tunapaswa kukubaliana ni MABADILIKO YA UENDESHAJI WA MPIRA NCHINI TANZANIA.
Nirudi katika klabu ya soka ya Yanga ambayo hapa ndio nayoiongelea. 
Tangu mwenyekiti Bw Yusuf manji achukue timu miaka 4 iliyopita kama mwenyekiti tumeshuhudia mabadiliko makubwa sana katika eneo moja kubwa ambalo ni kucheza mpira uwanjani katika hili yanga imefanikiwa sana kuliko timu nyingine yoyote ile naweza kusema hivyo hapa Tanzania, ukitazama mafanikio ya Yanga ubingwa mara 23 na katika mwaka uliopita kachukua kombe la ligi kuu , ngao ya jamii, na kombe la FA na pia amefanikiwa kucheza robo fainali kombe la shirikisho barani Africa.
Haya ni mafanikio makubwa sana ambayo yanga inapaswa kujivunia pamoja na mwenyekiti wao Bw manji.
Ukitazama timu inacheza mpira wa kisasa sana unaona mpira unavyoanza mpaka wanafunga goli mpira wa kufundishwa kisasa kabisaa na ndio mana hata katika michuano hii ya robo fainali ambayo inaendelea utaona u imara wa yanga kwa kucheza na timu kubwa ambazo zilishindwa kupata matokeo mazuri kwa yanga au kupata matokeo kiduchu kutokana na ubora wa timu ya Yanga mfano ni el ahaly, to mazembe, more bejaia na medeama ukiwauliza kuhusu yanga wao watakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kukuelezea ubora wa yanga.
JAMBO AMBALO YANGA HAIJAFANIKIWA MPAKA SASA NA AMBALO INAPIGANA NALO KAMA MGONJWA ALIEKO MAHUTUTI ICU NI UENDESHAJI WA KLABU.
Katika hili tangu kuanzishwa kwa yanga tumeshuhudia jitihada kubwa zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na yanga katika uendeshaji wa klabu tangu enzii za kina marehemu mzee tabu mangala, yusuf mzimba, wakaja kina jabir Katundu mpaka kwa marehemu abasi gulamali na george mpondela maarufu kana fidel castro walipambana sana na hili la uendeshaji wa klabu. 
Tukaja kushuhudia awamu ya msomi wa sheria Bw Tarimba abasi na suala la yanga kampuni na yanga asili haya yote yalikuwa ni mapambano ya mgonjwa aliekuwa MAHUTUTI akiangaika kupigania uhai wake hizo ni harakati nzuri sana na za kishujaa. 
Japo hazikuwezekana lakini tulijaribu vizuri sana na bado tutaendelea na hizi harakati.
SASA TUMEINGIA KWENYE MAPAMBANO MENGINE YA MANJI NA KUKODISHA CLUB 
Katika hili lazima kwanza tumpongeze Bw manji kwa kujaribu na kuthubutu nae kuanzisha mapambano ya kupigania uhai wa yanga katika kutafuta njia bora za uendeshaji wa klabu kwanza kwangu mimi huu ndio ujasiri wa mwanaume aliepitia Jandoni uamuzi wa kufufua tena uhai wa haya mapambano kwangu ni wa kishujaa sana Hongera mpambanaji manji na kwahili na wewe unaingia kwenye vitabu vya kihistoria vya yanga katika kupigania hili la mfumo wa uendeshaji wa klabu.
TUMUELEWE MANJI
Mambo ya biashara hayaendi kibubusa.Tumieni taaluma zaidi kuelewa kilichotokea Yanga.
Yanga SC 1935 haijauzwa wala haijakodishwa.
Kilichotokea: Mwekezaji anawekeza katika Yanga Football Team au Klabu ya soka ya Yanga (Ukumbuke Yanga SC inahusisha michezo mingi au shughuli nyingi).
Mwekezaji anawekeza katika kitu kinaitwa 1. "football team management contract" na 2.Anawekeza ktk "brand management contract"
Maana yake, mkataba utahusu 1.Uendeshaji wa Timu: kwa maana ya hiyo kampuni yake itaendesha timu ya soka ya Yanga na benchi lake la ufundi kwa gharama zao kuhusu masuala yote ya gharama za timu (usajili,mishahara,usafiri,posho n.k).
2.Mfadhili atatumia nembo ya Yanga kibishara kwa kuwekeza anavyowekeza iwe kuzalisha na kuuza jezi,vifaa vya michezo n.k na kuweka nembo ya Yanga.
Na katika namna zote mbili hapo juu.Yanga SC itavuna faida ya 25% (bila Yanga SC kuwekeza mtaji wowote bali value ya nembo na jina lake tu).
Katika mkataba wa aina hii maana yake Yanga SC itabaki na majengo yake, uongozi wake na itaendelea na masuala mengine ya Yanga SC huku ikiwa na hisa 25% ktk uendeshaji wa klabu na haitaumiza kichwa kuhusu usajili,mishahara wala huduma yoyote kwa team.
Katika kikao leo wanachama walitoa hoja ya kuongezwa kipengele cha pamoja na kuchukua team within hiyo 10 years mwekezaji pia awe ameboresha miundombinu kama uwanja wa mazoezi wa team etc.Inaelezwa hilo litajadiliwa kwa kina kati ya team ya mwekezaji na wachumi wa klabu.
Kuna hilo na masusla mengine ya kiufundi zaid Mkutano umeridhia kimsingi ila kati ya leo na j4 Baraza la Wadhamini na wataalamu wake litakamilisha majadiliano na kuingia mkataba.
Hii ndio arrangement ya kimkataba itavyokuwa na j4 value ya contract baada ya majadiliano itatangazwa.
JE KWA WATANI ZETU?
Sasa wazee wa Mooo tuambieni nyie juzi mmpepitisha "Safari ya Matumaini" tupeni details mmepitisha nini hasa na mfumo gani hasa wa kimkataba na Moooo!
Imeandikwa na mdau wa soka 
Jerry Cornel Muro 
0785333999

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video