Sunday, August 14, 2016

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema walikuwa na nafasi ya kuimaliza Mo Bejaia ya Algeria kwa mabao mengi zaidi.

Yanga jana imeichapa Mo Bejaia  bao 1-0 katika mechi ya Kombe la Shirikisho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Pluijm raia wa Uholanzi amekaririwa na Blog ya michezo ya Salehjembe akisema walikuwa na nafasi nyingi za kufunga, lakini hawakuzitumia.

"Tungezitumia, basi lingekuwa jambo jema sana. Lakini hatukufanya hivyo," alisema.

"Ninaamini tuna kikosi kizuri, lakini bado tunahitaji kurekebisha mambo kadhaa, pia hilo suala la umaliziaji," alisisitiza.

Goli pekee kwenye mchezo huo limefungwa na Amissi Tambwe dakika ya tatu akimalizia mpira uliotemwa na golikipa wa Bejaia Chamseddine Rahmani aliyeokoa mpira wa kichwa wa Simon Msuva.

IMG_0058
Katika mechi ya kwanza kabisa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi, Yanga ililala kwa bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Bejaia.

Hii ni mechi ya kwanza Yanga kushinda baada ya kucheza mechi tano, ikiwa imefungwa tatu, sare moja na kushinda moja ambayo ni ya leo.

Sasa Yanga ina pointi nne na inaendelea kubaki mkiani huku Bejaia inabaki na pointi tano sawa na Medeama ya Ghana huku TP Mazembe ya DR Congo ikiwa imejihakikishia kufuzu kwa kubaki kileleni na pointi 10.
Picha halisi kwa Yanga itaonekana baada ya matokeo ya mechi ya Medeama SC dhidi ya TP Mazembe inayotarajiwa kupigwa leo nchini Ghana.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video