Saturday, August 20, 2016

Simba imeuanza vyema msimu wa ligi kuu Tanzania bara kwa kupata ushindi wa magoli 3-1 mbele ya Ndanda FC ya Mtwara katika mechi ya kwanza ya msimu wa 2016/17 mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa taifa.

Mshambuliazi mpya wa Simba Laudit Mavugo alianza kuifungia klabu yake bao la kuongoza dakika ya 19 kipindi cha kwanza kabla ya bao hilo kusawazishwa na Omary Mponda dakika ya 36.

Timu zote zilikwenda mapumziko zikiwa sare kwa kufungana bao 1-1.

Baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji kwa kuwapumzisha wachezaji kadhaa na nafasi zao kuchukuliwa na wachezaji wengine.

Ndanda ilimpumzisha Aziz Sibo ambaye aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake ikachukuliwa na Bakari Mtama wakati Nassoro Kapama aliingia kuchukua nafasi ya Shija Nkiwa.

Simba wao waliwatoa Ibrahim Ajib ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Fredrick Blagnon, Mwinyi Kazimoto aliingia kuchukua nafasi ya Jamal Mnyate.

Fredrick Blagnon akaifungia Simba bao la pili dakika ya 74 kabla ya Shiza Kichuya kukamilisha ushindi kwa kukwamisha kambani bao la tatu.

Dondoo muhimu
  • Mavugo na Blagnon wamefunga magoli yao ya kwanza kwenye mechi ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara.
  • Goli la Mavugo ni la pili katika mechi tatu alizocheza akiwa Simba. Bao lake la kwanza lilikuwa kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, mechi ya pili ilikuwa dhidi ya URA ya Uganda ikiwa ni mechi ya pili ya kirafiki ya kimataifa.
  • Salum Telela amecheza mechi yake ya kwanza kama kwenye ligi akiwa nje ya Yanga tangu alipoachana na mabingwa hao watetezi wa VPL baada ya mkataba wake kumalizika.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video