Wekundu wa Msimbazi Simba SC baada mfululizo wa matokeo mazuri katika mechi zao za kirafiki, leo wamejikuta wakilala bao 1-0 kutoka kwa timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni KMC, mchezo ulifanyika mkoani Morogoro.
KMC walipata bao pekee katika mchezo wa leo kupitia kwa Rashidi Roshwa mnamo dakika ya 10 kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Emanuel Memba.
Simba, ambayo leo safu yake ya ushambuliaji ilikuwa ikiongozwa na Ame Ally 'Zungu' aliyetokea Azam kwa mkopo walikosa nafasi nyingi za wazi ambazo pengine zingeweza kubadili matokeo ya mchezo.
Simba wanatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kati ya kesho au keshokutwa tayari kujiandaa na mchezo dhidi ya ya FC Leorpads ya Kenya kuelekea siku ya maadhimisho ya Simba day, ambapo kilele chake ni Agosti 8.
0 comments:
Post a Comment