Sunday, August 14, 2016

Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo wamelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Wakusanya Ushuru wa Uganda URA, mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao Simba waliutumia kumuaga aliyekuwa nahodha wao Mussa Hassan 'Mgosi' ambaye amestaafu rasmi soka na kuwa meneja wa timu hiyo, URA ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 20 kupitia kwa Elikana baada ya kuunganisha krosi nzuri ambayo ilishindwa kuokolewa na mabeki wa Simba.
Simba, ambao walionekana kucheza soka la pasi nyingi na kasi walitulia na kufanikiwa kurejesha bao mnamo dakika ya 32 kupitia kwa Jonas Mkude, ambaye aliunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Mohammed Hussein Zimbwe Jr, baada ya Shiza Kichuya kufanyiwa madhambi hapo awali.

Kipindi cha kwanza
Takwimu za kipindi cha kwanza zilionesha timu hizo kuwa na nguvu iliyofanana ambapo, Simba alipiga mashuti yaliyolenga lango mawili, huku URA wakipiga matatu.
Mashuti yaliyotoka nje, kwa upande wa Simba walipiga 5, URA walipiga matatu, huku Simba wakipata kona tano na URA hawakuwa wamepata kona.
Simba walifanya madhambi mara 10, wakati URA walifanya faulo sita. Kwa upande wa kuotea (offside), kila timu iliotea mara moja.
Kadi ya njano, Simba walipata moja, huku URA hawakuwa wamepata. Kadi nyekundu hakuna timu iliyopata. Na upande wa umiliki wa mpira (ball possession), timu zote ziligawana asilimia 50 kwa 50.

Takwimu za mchezo mzima

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video