Saturday, August 6, 2016

Ikiwa ni siku 5 tangu kuanza kwa Simba Week, Klabu ya Simba leo hii imefanya usafi kwenye mtaa wa Msimbazi yaliko makao makuu ya klabu ya Simba. Zoezi la usafi lilihudhuriwa na mamia ya wanachama lilianzia mzunguko wa Msimbazi hadi kituo cha polisi Msimbazi.
Mgeni rasmi kwenye tukio hilo alikuwa Mbunge wa Ilala Mh Mussa Azan Zungu ambaye aliisifu Simba kwa kuwa klabu pekee kufanya shughuli za kijamii kama kufanya usafi, kuchangia damu, kugawa mipira, kliniki ya watoto na Simba week.
Viongozi wa Simba wakiongozwa na Makamu wa Rais Geofrey Nyange, Katibu Mkuu Patrick Kahemele, Msemaji wa Simba Haji Manara, Mjumbe wa kamati ya utendaji Iddi Kajuna na Mkurugenzi wa EAG Group Imani Kajula ambao ndio waandaaji wa Simba week na Simba Day.
Kilele cha Simba Day ni Jumatatu ambapo Simba itaumana na AFC Leopards.
Credit: Simba SC Tanzania

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video