Friday, August 19, 2016

Pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara linatarajiwa kufunguliwa rasmi wikiendi hii. Moja ya mechi zitakachozezwa ni Simba na Ndanda.

Msimu uliopita, katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 1-0 katika mchezo dhidi ya Ndanda, bao pekee lililofungwa na Ibrahim Ajibu. 

Katika mchezo wa raundi ya pili, Simba waliibuka tena washindi, safari hii wakiibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1, ambapo mabao yao yalifungwa na Hamisi Kiiza na Mwinyi Kazimoto katika Uwanja wa Taifa.

Hata hivyo Simba msimu uliopita hawakufanya vizuri sana baada ya kumaliza nafasi ya tatu na kukosa nafasi ya kuwakilisha taifa katika michuano ya kimataifa.

Msimu huu wameamua kufanya marekebisho makubwa kwenye bechi la ufundi na kumleta kocha Mcameroon Joseph Omog akishirikiana na Jackson Mayanja, ambaye msimu uliopita ndiyo alikuwa na majukumu ya kocha mkuu.

Watakuwa na kibarua kizito kuhakisha wanafanya vizuri msimu huu licha ya kusajili wachezaji wazuri, ambao watakuwa na msaada mkubwa.

Presha kubwa kwa Simba inakuja wakati ikielezwa kuwa, mshambuliaji wao mpya kutoka Burundi Laudit Mavugo bado hajapata leseni ya uhamisho wa kimataifa kumruhusu kucheza mechi za Ligi na hivyo kuukosa mchezo huo dhidi ya Ndanda.

Mavugo alionesha kiwango kikubwa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, ikiwa ni pamoja na kufunga goli zuri na kucheza tena vizuri kwenye mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya URA.

Taarifa zilizopo zinaeleza kwamba, tayari Katika Mkuu wa klabu hiyo Patrick Kahemele ameenda kulishughulikia suala hilo na kuhakikisha Mavugo anacheza haraka iwezekavyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video