Monday, August 8, 2016

 Katika kile kilichoonekana kupania kuwapa furaha mashabiki wao, Wekundu wa Msimbazi, Simba SC leo wamefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, pambano la Simba Day lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakionekana kutandaza soka la kitabu, Simba waliandika bao lao la kwanza dakika ya 38 kupitia kwa Ibrahim Ajibu Migomba baada ya kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa AFC Leopards.
Timu hizo zilienda mapumziko, huku Simba wakiwa na akiba ya bao moja mkononi.
Simba waliingia kipindi cha pili kwa kasi ya aina yake na kufanikiwa kuandika bao la pili kupitia kwa Ajibu tena baada ya kuunganisha krosi nzuri kutoka kwa Shiza Kichuya.
Kama haitoshi Simba waliandika bao tatu kupitia kwa Shiza Kichuya kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na mshambuliaji mpya Mburundi Laundit Mavugo baada ya kupiga krosi kutoka upande wa mashariki mwa uwanja.
Laudit Mavugo alihitimisha karamu ya magoli baada ya kuunganisha mpira uliopanguliwa na kipa wa AFC Leopards, kufuatia shuti kali lililopigwa na Shiza Kichuya kutoka pembeni mwa uwanja.
Simba leo walikuwa wakiadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa klabu yao na kufanya hafla kubwa uwanjani iliyoambatana na kulishana keki kwa baadhi ya viongozi wa timu hiyo.
Shughuli hii maalum ya Siimba Day hufanywa kila mwaka na mabingwa hao wa zamani wa Tanzania.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video