
"Nasikitika kwa kile kinachomtokea sasa," alisema Rummenigge katika mkutano na waandishi wa habari."Lakini hatujawa na wazo lolote la kumrejesha".
"Napenda kuwakumbusha kwamba Mwaka Mmoja uliopita, Bastian Schweinsteiger aliniomba mimi nimruhusu apate uzoefu mpya [kuhamia Manchester]," Alisema.
Schweinsteiger aliondoka Bayern na kujiunga na Man United majira ya kiangazi mwaka jana na alianza katika mechi 13 pekee akikipiga na Mashetani wekundu.
Wakati huu Manchester ipo chini ya Jose Mourinho, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ameripotiwa kufanya mazoezi na kikosi cha vijana chini ya miaka 23 na hii ni baada ya kuambiwa hana nafasi Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment