Thursday, August 4, 2016

Mbwana Samatta leo kwa mara nyingine tena atakuwa uwanjani, wakati timu yake ya KRC Genk itakapokuwa ikipambana na Cork City F.C katika mchezo wa marudiano wa arundi ya tatu ya mchujo kufuzu kucheza Ligi ya Europa msimu huu utakaoanza hivi karibuni.
Genk, ambao leo watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Turner's Cross, mjini Cork huko nchini Ireland watahitaji ushindi au sare yoyote ili kuweza kufuzu kufuatia mchezo wa awali kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 Alhamisi ya wiki iliyopita.
Kabla ya kukutana na Cork City F.C, Genk waliwang'oa Buducnost ya Montenegro baada ya kushinda kwa penalti 4-2, kufuatia kutoshana nguvu kwa wastani wa mabao 2-2.
Katika hatua hiyo ya mikwaju ya penati, Samatta pia alifanikiwa kuifungia timu yake penati, ambayo ilikuwa chachu ya ushindi kwenye mchezo huo.
Baada ya hatua hii, timu zitaibuka na ushindi zitakwenda hatua ya mwisho ya mchujo na baada ya hapo tena zitafuzu moja kwa moja hatua ya makundi, ambapo watakumbana na miamba ya soka kama Manchester United ambao wataanzia kwenye hatua hiyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video