Tuesday, August 30, 2016

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea timu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta anatarajiwa kuungana na timu hiyo nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).

Hadi mchana wa leo Agosti  29, 2016 ni Kelvin Yondan pekee kutoka Young Africans ambaye hakuripoti kwenye kikosi hicho kilichopiga kambi yake kwenye Hoteli ya Urban Rose iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam. Kipa mpya wa timu hiyo, Said Kipao alijiunga na timu hiyo mara moja baada ya kuteuliwa na Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa.

Taifa Stars inatarajiwa kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles utakaofanyika Septemba 3, 2016. Licha ya mchezo huo kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.

Wachezaji wanaotarajiwa kuondoka ni:

Makipa-

Said Kipao – JKT Ruvu

Aishi Manula – Azam FC



Mabeki

Kelvin Yondani - Young Africans

Vicent Andrew - Young Africans

Mwinyi Haji - Young Africans

Mohamed Hussein – Simba SC

Shomari Kapombe - Azam FC

David Mwantika - Azam FC



Viungo

Himid Mao - Azam FC

Shiza Kichuya – Simba SC

Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar

Jonas Mkude – Simba SC

Muzamiru Yassin – Simba SC

Juma Mahadhi - Young Africans

Farid Mussa Tenerif ya Hispania


Washambuliaji

Simon Msuva - Young Africans

Ibrahim Ajib – Simba SC

John Bocco - Azam FC


Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video