Tuesday, August 9, 2016

Bosi wa Real Madrid, Zinedine Zidane amemtakia kila la kheri Paul Pogba katika maisha yake ya soka ndani ya Manchester United.
Real Madrid ilikuwa inahusishwa kumsajili Pogba, lakini ilijitoka katika mbio hizo na kuwaacha wakali wa Old Trafford waendeleze mchezo na hatimaye wameukamilisha.

Akikaririwa na Gazeti la Mundo Deportivo, Zidane alikuwa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mechi ya leo ya UEFA Super Cup akikabiliana na Sevilla mjini Oslo Norway, Gwiji huyo wa Ufaransa aliulizwa mtazamo wake juu ya usajili wa Poga.

"Siwazi chochte. Pogba ni mchezaji wa Manchester United na ndivyo ilivyo. Namtakia kila la kheri, hakuna zaidi". Amesema Zizou.
Zidane sio mgeni wa mambo ya kuvunja rekodi katika usajili kwani Real Madrid walivunja rekodi ya Dunia mwaka 2001 wakimsajili yeye kwa ada ya paundi milioni 46 kutokea Juventus ya Italia na tayari wakati huo alikuwa ameshinda Ubingwa wa Ulaya na kombe la Dunia.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video