Tuesday, August 30, 2016

Hassan Kessy (Kulia)

Suala la beki Hassan Kessy limechukua sura mpya baada ya kuanza kusikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, lakini imeelezwa kwamba litapangiwa siku nyingine.

Blog ya michezo ya Salehjembe imeripoti kuwa kamati hiyo ilikaa jana na kuwajumuisha viongozi mbalimbali wa Simba pamoja na wale wa Yanga ambao walitoa utetezi wao.

Taarifa zinaeleza, Simba imewasilisha ushahidi wake ambao unaonesha kuwa Kessy alijiunga na Yanga kabla ya mkataba wake kwisha.

Suala hilo linamfanya Kessy awe amevunja mkataba na kulazimika kuangalia nini kinatakiwa baada ya kuvunja mkataba.

Tayari TFF imemruhusu Kessy kuendelea kucheza wakati kamati hiyo ikiwa ndiyo imeanza kusikiliza kesi hiyo.

Simba wamekuwa na uhakika kama watafanya vizuri katika kesi hiyo kwa kuwa wana vielelelezo kwamba alivunja mkataba kusaini mkataba mwingine na Yanga wakati hajamaliza wakwao.

"Kweli Simba wamewasilisha ushahidi wao na inaonekana ni kama kila kitu kipo vizuri, sasa hatujui itakuwaje, vizuri tuache suala hilo lishughulikiwe baadaye," kilieleza chanzo.
Kama Kessy atapatwa na hatia ya kuvunja mkataba, kwa mujibu wa kipengele cha kuvunja mkataba wake na Simba , atatakiwa kulipa fidia ya dola 600,000/=


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video