Karl-Heinz Rummenigge amerusha lawama zake kwa klabu ya Manchester United na Jose Mourinho kwa namna wanavyomtendea nyota wa zamani a Bayern Munich Bastian Schweinsteiger.
Schweinsteiger, ambaye amewahi kutwaa Kombe la Dunia na Ujerumani, hivi karibuni alitangaza kustaafu soka la kimataifa punde tu baada ya Ujerumani kutolewa katika hatua ya nusu fainali kwenye Michuano ya Euro mwaka huu, amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake huku klabu ikisema hayuko kwenye mipango yao.
Rummenigge ameshtushwa na taarifa za Schweinsteiger kuondolewa kwenye kikosi cha Manchester United huku taarifa zikieleza zaidi kwamba kwa sasa mkongwe huyo anafanya mazoezi na kikosi cha vijana.
Mwenyekiti Mtendaji huyo wa Bayern anaamini kwamba kitendo hicho alichofanyiwa Bastian kitawashtua wachezaji wengi wakubwa na kufikiria mara mbili-mbili kujiunga na klabu hiyo.
"Wakati niliposoma taarifa ile nilipata wakati mgumu sana kuamini," Rummenigge alinukuliwa na Bild.
"Mchezaji mmoja au wawili lazima wajifikirie zaidi kama kweli watakuwa sahihi kwenda katika klabu ile.
"Kitu kama hicho hakijawahi kutokea hapa Bayern Munich na kamwe hakitatokea."
0 comments:
Post a Comment