Wednesday, August 17, 2016


Leicester City wametangaza kumsainisha mkataba mpya wa miaka minne winga wao Riyad Mahrez.

Kwa kipindi kirefu Mahrez, 25, amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia klabu ya Arsenal, lakini kwa sasa dili hilo limeota mbawa.

Winga huyo wa kimataifa wa Algeria amefuata nyayo za mshambuliaji Jamie Vardy, ambaye pia awali alihusishwa kujiunga na Arsenal kabla ya kuongeza mkataba mpya klabuni hapo.
Msimu uliopita, Mahrez aliifungia Leicester mabao 17 na kutoa pasi za magoli 11 na kuisaidia timu hiyo kutwaa ndoo ya EPL.

Mahrez ambaye alifunga goli pekee wakati Leicester ilipofungwa mabao 2-1 na Hull City kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi ya England, msimu uliopita alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka.

Awali kabla ya kusaini mkataba mpya, Mahrez alisema ni klabu mbili au tatu duniani ndizo angeweza kujiunga nazo endapo zingemhitaji.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video