Yanga yatakiwa kufanya haraka kuwasilisha usajili wake |
KLABU ya Yanga na timu nyingine ambazo zilichelewa kuwasilisha usajili Shirikisho la Soka Duniani FIFA, sasa mambo yamewanyokea baada ya FIFA kukubali utetezi wao na kuamua kuwafungulia dirisha la usajili TMS.
Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas imeithibitisha MPENJA SPORTS asubuhi hii kwamba, maamuzi hayo ya FIFA yamefikiwa baada ya timu hizo kutoa maelezo ya kwanini zilichelewesha usajili, lakini TFF pia imetoa hoja nzito za kuzibeba timu zake ambazo zilikuwa hatarini kushushwa daraja.
"Kwa kifupi ni kwamba tulizitaka klabu ndani ya siku mbili zilizopita, bila shaka utakumbuka ilikuwa Jumanne na Jumatano. Tuliwaambia waandike barua ya kujitetea au kutoa sababu kwanini hawakukamilisha usajili mapema.
, klabu zimefanya hivyo". Amesema Lucas na kusisitiza: "Kwa kuongezea maelezo na hoja nzito za TFF kulingana na mazingira tuliyokuwa nayo huku Tanzania na kasi ya mtandao, tumekubaliwa na FIFA ili tuondokane na adhabu ya aina yoyote, wao wamefungua".
Hata hivyo, Lucas amesema inabidi Yanga iharakishe usajili wake kwani ifikapo kesho saa 6:00 usiku FIFA itafunga TMS.
"Sasa ninavyozungumza na wewe, ni kwamba tayari wamefungua kuanzia saa sita kamili usiku wa kuamkia leo mpaka kesho saa sita kamili usiku wa kesho".
"Jambo hili kulitekeleza kama timu ina nyaraka zote haliwezi kuchukua hata saa tatu, wakianza sasa hivi yawezekana saa nane au tisa Alasiri wanaweza wakawa wamemaliza, lakini kama watajenga dhana ile ile kwamba nitafanya baadaye au nitafanya kesho itawagharimu, zaidi ya hapo sina maelezo nini kitatokea" . Ameeleza Alfred Lucas.
Lucas imesema kama Yanga au timu yoyote itashindwa kukamilisha hilo, basi wafike TFF ambako watasaidiwa bure.
"Ndio maana tuliita mafunzo kwa Maneneja wa timu waje wajifunze mfumo wa TMS, Yanga hawakuja (katibu mkuu), kama hawana mtu yeyote anayeweza kuwasaidia, wamfuate meneja wa TMS, Jonas Kiwia , TFF tutafanya kazi hiyo bure kwa ajili yao". Amefafanua Msemaji huyo.
0 comments:
Post a Comment