Paul PogbaMlinzi wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand amesema klabu hiyo kwa gharama yoyote ile inatakiwa kumrejesha Old Trafford, Paul Pogba kutoka Juventus ya Italia. |
"Haijalishi watu wanasemaje kuhusu ada ambayo Juventus watapata kwa kumuuza Paul Pogba kwasababu hicho ndicho kiwango kinachostahili kwa mchezaji wa hadhi yake," Amesema Ferdinand ambaye sasa ni mchambuzi wa soka BT Sport.
"Sio muda mrefu sana watu walikuwa wanasema United haitumii pesa za kutosha, kwahiyo sasa nasema watumie na wampate Pogba kwa gharama yoyote ile". Amefafanua Ferdinand.
Hata hivyo, Ferdinand ametofautiana na kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Schores ambaye siku za karibuni alikaririwa akisema, Pogba ni mchezaji mwenye thamani kubwa, lakini hawezi hastahili Paundi milioni 100 ambazo United wanataka kulipa.
Kama United wanaoripotiwa kukaribia kukamilisha usajili wa Pogba watalipa kiasi hicho cha fedha basi watavunja rekodi ya dunia.
0 comments:
Post a Comment