Nyota ya Zinedine Zidane imezidi kung'aa baada ya usiku wa kuamkia leo kushuhudia timu yake ya Real Madri ikimpata taji la pili tangu akabidhiwe timu hiyo baada ya kuwachapa Sevilla mabao 3-2 kwenye mchezo wa UEFA Super Cup uliochezwa knako Uwanja wa Lerkendal nchini Norway.
Real Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 huku bao la ushindi la Dani Carvajal likifungwa dakika 11 kabla ya dakika 120 kukatika.
Real Madrid ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa chipukizi wao Marco Asensio dakika ya 21.
Sevilla wakaja juu na kusawazisha bao kupitia kwa nyota wao Franco Vazquez mnamo dakika ya 41, ikiwa ni dakika chache tu kabla ya kwenda mapumziko.
Sevilla kwa mara nyingine tena waliandika bao la kupitia kwa Yevhen Konoplyanka kupitia mkwaju wa penati Ramos kumuangusha Vitolo, huku zikiwa zimesalia dakika 18 mchezo kumaliza.
Ramos alisawazisha makosa yake kufuatia kuifungia Madrid bao la pili na la kusawazisha mnamo dakika ya 90 na kufanya mchezo huo kwenda dakika 120.
Kwenye dakika hizo 30 za ziada, Real Madrid walipata bao la tatu na la ushindi mnamo dakika ya 119 kupitia kwa Dani Carvajal na kufanikiwa kuchukua ndoo hiyo ya Super Cup.
0 comments:
Post a Comment