Wednesday, August 3, 2016

 Makamu wa Rais wa Simba, Nyange Kaburu (kushoto) akiwa na Mvugo

SIKU moja baada ya Mfanyabiashara maarufu nchini na Mwanachama wa Simba SC, Mohamed Dewji 'Mo' kuichangia klabu hiyo milioni 100 za usajili, hatimaye wamefanya dili la maana kwa kumleta  mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo.


Mavugo ambaye ametokea nchini Ufaransa alikokwama  kujiunga na klabu ya Tours ya Ligi Daraja la Pili, Ufaransa maarufu kama Ligue 2 ametua usiku huu jijini Dar es salaam kuja kumalizana na Wekundu hao wa Msimbazi wenye agenda nzito ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji unaosukumwa zaidi na MO.
Straika huyo ambaye amezungumzwa kwa muda mrefu kujiunga na Simba na kufikia hatua watani zao wa jadi kuanza kuwatania kwa jina la 'Wazee wa Mavugo' amepokelewa na makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.
Katibu mkuu wa Simba, Patrick Kahemele ameithibitisha MPENJA SPORTS usiku kuwa Mavugo ameshatua.


Inaonekana Mavugo atakuwa akivaa jezi namba 45 mara atakapokamilisha usajili wake, bahati nzuri uhakika upo kutokana na mkwanja aliomwaga MO.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video