Tuesday, August 16, 2016

Ni kitu kigumu sana kutokea hasa kwa vyombo vya habari vikubwa nchini England kuchapisha habari ambayo ina ukakasi ndani yake au habari ambayo siyo ya kweli kuhusu mchezaji.

Andrea Pirlo amefichua kitu ambacho, Daily Mail wamekifanya kwake wakati walipochapisha habari ambayo, yeye binafsi anasema aliongea kama utani tu juu ya kitendo cha Manchester United kumwachia Pogba aondoke free na kujiunga na Juventus ya Italy.

Gazeti la Daily Mail lilimnukuu Pirlo akisema: ‘Kwenye siku ya kwanza kabisa ya mazoezi ambapo Pogba alihudhuria akiwa kama mchezaji wa Juventus, wachezaji wengi walicheka sana,’

‘Hatucheki kwasababu yoyote nyingine zaidi ya kutoamini kwamba, mchezaji huyu mwenye uwezo unaojidhihirisha ameruhusiwa kuondoka bure kwenye klabu kubwa kama Manchester United, na nadhani Juventus bado wanacheka.

‘Wakati tunarudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kumaliza muda wa mazoezi nakumbuka vizuri tu Gianluigi Buffon alivyonifuata na kuanza kucheka na kusema : “Hivi ni kweli wamemruhusu aondoke bure tu?”

‘Walimsajili mchezaji mwenye uwezo mkubwa bila kiasi chochote cha fedha, alikuwa ni sehemu muhimu sana ya timu iliyoshinda makombe ndani ya miaka minne, halafu wamemuuza kwa paundi mil 90. Kwa namna yoyote utakavyoliangalia suala hili, Juventus wamelamba dume.’ 

‘Ni mchezaji bora kijana miongoni mwa niliowahi kuwaona, na sidhani kama tutakosea kumwita mchezaji bora wa dunia. Kwa muda mrefu sana imekuwa ni Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, lakini sasa tasnia ya soka ikae tayari kumpokea mfalme mwingine.

Pirlo akanusha kupitia Instagram yake.
Akionekana mwenye hasira baada ya kuona maneno hayo yamechapishwa kwenye gazeti huku yakimnukuu, Andrea Pirlo ameamua kuandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Instagram kujibu mapigo kwa Daily Mail.

Pirlo (37) ambaye anakipiga kunako klabu ya New York City FC ameweka picha ambayo yenye maandishi yanayosomeka “Caution: No bulls*** zone” na chini kuweka maelezo yanayosomeka “Just to make it clear, I never gave any interview to the daily mail talking about Pogba and Manchester.”

Tahadhari sina nafasi kwa mambo ya kipuuzi......."Nataka kuwafahamisha kwamba, sikuwahi kufanya mahojiano yoyote na daily mail kuhusu Pogba na Manchester."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video