Nyota wa Manchester United aliyesajiliwa kwa pesa iliyovunja rekodi ya dunia Paul Pogba amesimamishwa kucheza mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya England, hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na FA.
Pogba, 23, amesajiliwa na United kutoka Juventus kwa ada ya paundi mil 89.3, ikiwa ni miaka minne tu imepita baada ya kuondoka klabuni hapo ambapo alinunuliwa kwa paundi 800,000.
Hata hivyo, itamlazimu Pogba kukosa mchezo dhidi ya Bournemouth Jumapili na kusubiri mchezo wa pili.
Pogba amesimamishwa kucheza mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano ambazo alizipata katika mchezo wa fainali ya pili ya Copa Italia dhidi ya AC Milan.
0 comments:
Post a Comment