Wednesday, August 17, 2016

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane leo amepata jeraha baya la bega na kukimbizwa hospitalini haraka kufuatia kuumizwa mazoezini na beki wa kushoto wa timu hiyo Alberto Moreno.

Mane ambaye amesajili kwenye majira haya ya kiangazi kwa paundi mil 30 akitokea Southmpton, ameonesha kiwango kikubwa kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Arsenal na kufanikiwa kufunga goli la nne wakati Liverpool ikiibuka na ushindi wa mabao 4-3 katika uwanja wa Emirates.

Kuumia kwa Mane kutakuwa ni pigo kubwa kwa Liverpool hasa ukizingatia kwamba, Msenegali huyo amekuwa ni kipenzi kikubwa cha kocha Jurgen Klopp. 

Inaarifiwa kuwa, endapo Mane atathibitika kuteguka bega lake basi atakaa nje kwa miezi mingi, hivyo kuzua hofu kwa mashabiki wa Liverpool.

Mechi inayofuata kwa Liverpool ni hapo Jumamosi ikiwa ni Ugenini tena na Burnley, na hii ni Mechi yao ya pili mfululizo kucheza Ugenini kwenye Ligi Kuu England na hilo ni kwa makusudi tu kutokana na maombi yao wenyewe ili kupisha ujenzi wa upanuzi wa Jukwaa Kuu la Uwanja wao wa Anfield.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video