Sunday, August 7, 2016

MECHI YA Ufunguzi Pazia la Msimu Mpya wa ligi kuu soka ya England inachezwa leo kuanzia majira ya saa 12:00 Jioni kwa saa za Afrika Mashariki ambapo Mabingwa wa England na wale waliobeba FA CUP wanakutana kugombea Ngao ya Jamii Uwanjani Wembley Jijini London.
Mechi hii inawakutanisha Leicester City ambao ni Mabingwa wa England na Manchester United Mabingwa wa FA CUP.
Awali Taji hili lilikuwa likiitwa Ngao ya Hisani lakini sasa ni Ngao ya Jamii na hii ni mara ya 94 kushindaniwa na Mdhamini wake Mkuu ni McDonald ambao ni maarufu kwa Hoteli za Vyakula vya Hamburger Duniani kote.
Mara ya mwisho kukutana, Timu hizo zilitoka 1-1 Msimu uliopita kwenye mechi ya Ligi Kuu England ambayo Leicester walitanguliwa kufungwa kwa Bao la Anthony Martial na kusawazisha kupitia Wes Morgan.
Siku moja baada ya Mechi hiyo, Leicester wakatwaa Ubingwa baada ya Wapinzani wao Spurs kutoka Sare na Chelsea huko Stamford Bridge.
Hilo lilikamilisha Msimu wa ajabu kwa Leicester baada ya Msimu mmoja uliopita, ule wa 2014/15 chupuchupu kunusurika kushushwa Daraja.
Lakini chini ya Meneja Claudio Ranieri Msimu wa 2015/16 walibadilika na kushangaza wengi kwa kutwaa Ubingwa wao wa kwanza katika Historia yao.
Ranieri ndie alikuwa Meneja wa Chelsea kabla Jose Mourinho hajatua huko kumbadili.
-Man United wametwaa Ngao ya Jamii mara 20, ikiwa ni mara 5 zaidi ya Timu inayowafuata [Liverpool mara 15].
Hali za Timu
Mabeki wa Manchester United Chris Smalling na Timothy Fosu-Mensah, ambao walikuwa Majeruhi sasa wako fiti na huenda wakashiriki Mechi hii.
Wachezaji wapya wa Man United Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan na Eric Bailly huenda nao wakaanza Mechi hii.
MAN UNITED-Timu itatokana na Kikosi hiki:
De Gea, Romero, Bailly, Jones, Rojo, Darmian, Fosu-Mensah, Valencia, Smalling, Blind, Shaw, Carrick, Herrera, Schneiderlin, Fellaini, Lingard, Young, Mata, Mkhitaryan, Depay, Martial, Rooney, Rashford, Ibrahimovic.
Kwa upande wa Leicester City, Wachezaji wao wapya Ahmed Musa, Papy Mendy na Luis Hernandez huenda wakaanza pamoja na wengine wapya Ron-Robert Zieler na Bartosz Kapustka.
LEICESTER CITY-Timu itatokana na Kikosi hiki:
Schmeichel, Zieler, Chilwell, Schlupp, Morgan, Hernandez, Wasilewski, Huth, Fuchs, Simpson, Kapustka, Gray, Amartey, King, Mendy, Drinkwater, James, Albrighton, Mahrez, Ulloa, Okazaki, Musa, Vardy.
REFA: CRAIG PAWSON
LIGI KUU ENGLAND
Msimu Mpya 2016/17
Ratiba:
Jumamosi Agosti 13
Saa za Afrika Mashariki
1430 Hull City v Leicester City
1700 Burnley v Swansea City
1700 Crystal Palace v West Bromwich Albion
1700 Everton v Tottenham Hotspur
1700 Middlesbrough v Stoke City
1700 Southampton v Watford
1930 Manchester City v Sunderland
Jumapili Agosti 15
1530 A.F.C. Bournemouth v Manchester United
1800 Arsenal v Liverpool
Jumatatu Agosti 16
2200 Chelsea v West Ham United

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video