Tuesday, August 2, 2016

Lile sakata la Mfanyabiashara maarufu na Mwanachama wa Simba SC, Mohamed Dewji 'MO' kutaka kuinunua klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa linazidi kunoga baada ya mchana wa leo kukabidhi kwa Rais wa Simba, Evans Aveva Shilingi za Kitanzania Milioni 100 ili kusaidia usajili wa wachezaji.
MO ametoa kitita hicho kwenye mkutano na waandishi wa habari ambao Aveva aliongozana na katibu mkuu wa Simba, Patrick Kahemele.
Hata hivyo fedha hizo ni nje ya Ofa ya Bilioni 20 aliyoweka mezani akitaka hisa asilimia 51, huku akitaka mchakato wa kuibadili Simba kwenda kampuni kukamilika si zaidi ya miezi mitatu ijayo.
Jana, uongozi wa Simba ulimuandikia barua kumuomba Mo atoe fedha za usajili kama alivyoahidi kusaidia wakati akitangaza nia yake ya kutaka kununua asilimia 51 za klabu ya Simba.


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video