Leo Messi aliishangaza Dunia na Taifa lake la Argentina pale alipotangaza kustaafu Soka la kimataifa kufuatia nchi yake kupoteza fainali ya Copa America mwaka huu.
Nyota huyo wa Barcelona alikerwa na Argentina kuchapwa fainali tatu akiichezea timu hiyo na aliona hakuna haja ya kuendelea kuitumikia kwa maumivu yasiyoisha.
Maamuzi ya Messi yaliwaumiza Wargentina wengi na wote akiwemo Rais wa Nchi, walimtaka arejee timu ya Taifa
Sasa habari rasmi zinasema Messi amekubali kurejea timu ya Taifa.
Chama cha Soka cha Argentina kimetangaza kuwa nahodha huyo ameamua kurudi kama alivyoombwa na atakuwepo kwenye kikosi kijacho kitakachocheza mechi za kuwania kufuzu kombe la Dunia 2018.
Taarifa rasmi ya Chama cha Soka cha Argentina (AFA) juu ya kurejea kwa Messi
0 comments:
Post a Comment