NYOTA wa Medeama ya Ghana, Victor Storey, amesema aliitazama Yanga, walipocheza nayo akabaini kwamba kikosi chao ni imara ila kinapungukiwa na upambanaji ndani ya dakika 90.
“Hakuna timu ambayo inakosa mapungufu ila wakilifanyia kazi suala la kujitolea kwa ajili ya timu ndani ya dakika 90, wanaweza wakafika mbali na kufanya makubwa Ukanda wa Afrika kwani kila kitu ni dhamira ya dhati ndipo mafanikio utayaona,” aliiambia Mwanaspoti
“Pia nimeona tatizo wakifungwa ni kama wanakata tamaa ya kupambana ila ukweli Yanga, ipo vizuri na ina nyota ambao ukiwatazama wanaweza wakafika mbali zaidi ya pale walipo kwa sasa,” aliongeza.
Alipoulizwa kama akipata ofa atapenda kucheza timu gani alijibu: “Nilivyoifahamu kiundani ni Yanga, ingawa tulipokuja Tanzania, tumesikia habari za Simba, soka la Tanzania lina ushindani ambalo litamfanya mchezaji makini aweze kufikia ndondo zake kirahisi, nikipata ofa nitacheza timu inayohitaji huduma yangu,” alifafanua.
0 comments:
Post a Comment