Baba Rahman ajiunga na Schalke
Mambo hayakuwa mazuri kwa Baba Rahman kunako klabu ya Chelsea.
Beki huyo wa kushoto wa mwenye asili ya Ghana msimu uliopita alijiunga na Chelsea akitokea klabu ya Augsburg kwa ada ya paundi mil 14.
Ilitumainiwa kwamba Rahman angependa vizuri sana Chelsea katika nafasi ya beki wa kushoto, hata hivyo imekuwa kinyume chake baada ya kushindwa kabisa kuonesha makali katika msimu wake wa kwanza kwa wababe hao wa darajani.
Mashabiki wengi wa Chelsea walimshutumu Baba Rahman kwamba hakuwa na uwezo wa kuichezea klabu hiyo
Mwishoni mwa wiki hii, taarifa zilianza kuenea kwamba Baba Rahman alikuwa akiwaniwa na Schalke, na jana dili lake la kujiunga na klabu hiyo lilikamika rasmi.
Baba ameondoka Chelsea kwa mkopo
Baba Rahman amejiunga na Wajerumani hao maarufu kwa jina la Royal Blues kwa mkopo wa msimu mzima.
Mapema jana asubuhi, beki huyo wa Chelsea alifanyiwa vipimo vya afya kwaajili ya kujiunga na klabu hiyo.
Baba Rahman alichezea Chelsea michezo 23 tu msimu uliopita kwenye michuano yote.
0 comments:
Post a Comment