Wakati huu nyaraka za usajili wake wa Paundi milioni 100 zikithibitishwa kuwasili nchini England, kiungo wa Ufaransa na Juventus, Paul Pogba ameendelea kujiweka fiti huko Marekani kuelekea msimu mpya 2016/2017.

Dili la Pogba kujiunga na Manchester City linatarajiwa kutangazwa siku yoyote kutoka sasa, lakini nyota huyo anaendelea na likizo yake ya majira ya kiangazi mjini New York ambapo jana alionekana akifanya mazoezi ya kupigana ngumi 'kickboxing' .
Pogba ame-post video kwenye akaunti yake ya Twita akimuonesha akipangua ngumi na kumpiga mateke mpinzani wake, huku akiwa amevaliwa vest ya nyota wa Golden State Warriors, Stephen Curry.
Pogba, 23, anarejea Man United kwa dau linaloweka rekodi mpya ya Dunia, ingawa bado kuna mjadala mzito kama kiungo huyo ana thamani hiyo ya paundi milioni 100.
0 comments:
Post a Comment