Friday, August 12, 2016

 Mabingwa wa Soka Tanzania bara, kesho Jioni uwanja wa Taifa,  Dar es salaam watashuka dimbani kukabiliana na MO Bejaia ya Algeria katika mchezo wa nne wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.  
Kuelekea katika mechi hiyo, Katibu mkuu wa Yanga SC, Baraka Deusdedit amesema maandalizi yote yamekamilika na wachezaji wapo kwenye ari kubwa ya kutafuta pointi tatu.
"Kiujumla kila kitu kinaendelea vizuri, niahidi tu kwamba maandalizi tunayofanya ni ya kwenda kupambana kutafuta pointi tatu . Vijana wana ari,  wanafanya mazoezi kwa utashi mkubwa wakihitaji pointi tatu". Amesema Deusdedit na kuongeza: "Tiketi zitauzwa siku hiyo hiyo ya mchezo (Kesho), kiingilio cha chini ni 3000/- na cha juu kabisa ni 15000/-".
Aidha, Deusdedit amewaomba mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo.
"Niwaombe mashabiki wajitokeze kwa wingi, waipe sapoti timu yetu, waipe shamrashamra uwanjani, niwaahidi tushikame, tusali pamoja, tuweze kupata pointi tatu". Alifafanua Mtendaji huyo mkuu wa Yanga.
Kwa upande wa kocha mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm alisema timu yake haijakata tamaa katika michuano Kombe la Shirikisho.

Pluijm alieleza kuwa bado wanapambana na watakachofanya ni kuibuka na ushindi dhidi ya Bejaia ambayo iliwafunga bao 1-0 kwao Algeria.

“Mechi itakuwa ngumu, lakini katika soka hauwezi kukata tamaa mapema tena kwa rahisi namna hiyo. Kama tutashinda, basi tuna nafasi bado,” alisema Pluijm.


Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja huo leo kabla ya mechi hiyo ya Jumamosi.
Licha ya kwamba Young Africans kuwa na pointi moja, bado ina nafasi ya kushika nafasi za juu katika kundi la A ambalo msimamo wake unaongozwa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku Mo Bajaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, zina pointi tano kila moja. Wakati Young Africans wanacheza na Mo Bajaia iliyoshinda mchezo wa kwanza huko Algeria, Medeama itakipiga na TP Mazembe.
 Mchezo wa Young Africans dhidi ya Mo Bajaia utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia ambako katikati atakuwa Bamlak Tessema Weyesa akisaidiwa na Kindie Mussie mstari upande wa kusini na Temesgin Samuel Atango katika mstari wa Kaskazini upande wa wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Haileyesus Bezezew Belete.
Kamishna wa mchezo atakuwa Gaspard Kayijuka kutoka Rwanda wakati Desire Gahuka wa Burundi atasimamia ufanisi wa waamuzi wa mchezo na Mratibu Mkuu wa mchezo atakuwa Isam Shaaban kutoka Sudan. Mratibu huyo anatarajiwa kuwasili leo Agosti 10, 2016 wakati waamuzi watatua kesho Agosti 11, 2016 na msimamizi wa waamuzi atatua Ijumaa Agosti 12, 2016.
Kiingilio katika mchezo huo kitakuwa ni Sh 3,000 kwa mzungunguko kwa maana ya viti vya kijani, bluu na chungwa wakati Viti Maalumu vyenye hadhi ya daraja B na C kiingilio kitakuwa Sh 10,000 wakati A kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 kwa mujibu wa Waratibu wa Young Africans.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video