Saturday, August 20, 2016

Zlatan Ibrahimovic amefunga mabao mawili akiicheza kwa mara ya kwanza kwenye dimba la Old Trafford kama mchezaji wa Manchester United na kuzidi kuisogeza timu hiyo kileleni zaidi.

Msweden huyo alifunga goli la kwanza baada ya kupokea krosi maridhawa iliyochongwa kutoka upande wa kulia na Wayne Rooney.

Zlatan alifunga bao la pili kwa njia ya penati baada ya beki wa kushoto wa Man United Luke Shaw kufanyiwa madhambi na Jordy Clasie.

Paul Pogba, ambaye amesajili kwa paundi mil 89 kutoka Juventus kwa mara ya kwanz leo ameichezea klabu hiyo na kuonesha uwezo mkubwa sana.

Dondoo muhimu 

  • Zlatan Ibrahimovic amefunga magoli 13 kwenye michezo 8 iliyopita ya ligi dhidi ya timu zilizofundishwa na Claude Puel - akifanya hivyo pia wakati akiwa Paris St-Germain dhidi ya Nice.
  • Magoli matatu kati ya sita ya Zlatan amefunga kwa njia ya kichwa.
  • Manchester United hawajapoteza mchezo wowote wa ligi ambao wameongoza mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika tangu Mei mwaka 1984.
  • Paul Pogba leo amecheza kwa mara ya kwanza kama mchezaji wa Manchester United tangu March 18 mwaka 2012, sawa na siku 1,616 zilizopita.
  • Wayne Rooney amecheza mchezo wake wa 600 kwenye mechi ya leo (michezo 523 akiwa na Man United na 77 akiwa na Everton).
  • Manchester United hawajapoteza mchezo wowote waliocheza Ijumaa tangu mara ya mwisho walivyofungwa 2-0 na mwaka 1950 Birmingham. Wameshinda mara 14 na kutoka sare mara sita.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video