Sunday, August 14, 2016

 Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wanatarajia kujipima nguvu dhidi ya URA FC ya Uganda katika mechi ya Kimataifa ya kirafiki inayotarajia kuchezwa leo uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Mtanange huo wa pili wa kimataifa wa kirafiki kwa Simba kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Agosti 20, utaanza saa 10:00 Jioni.
Mshambuliaji Laudit Mavugo aliyefunga bao moja, Ibrahim Hajib aliyepachika mawili na Shiza Kichuya aliyefunga moja kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya AFC Leopard katika Tamasha la Simba Day wanasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Simba wanaoamini sasa wamerejea kwa makali.
Pia huu ni mchezo maalum kwa Wanasimba kwasababu utatumika kumuaga rasmi Nahodha na Mshambuliaji Mkongwe wa klabu hiyo, Mussa Hassan Mgosi anayestaafu Soka leo.
Baada ya mechi hiyo, Mgosi atakabidhiwa rasmi majukumu ya kuwa Meneja wa Simba.
Matukio haya yote yamethibitishwa kuwa Live kupitia AZAM TWO na AZAM SPORTS HD.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video