Usiku wa kuamkia leo, Usain Bolt ameshinda mbio za mita 200 kwenye Michuano ya Olimpiki Rio 2016 na kubeba medali ya dhahabu na kufanya awe na jumla ya medali nane za dhahabu tangu alipoanza kushiriki michuano hiyo. Bolt sasa ameweka hai matumaini yake ya kushinda medali tatu za dhahabu.
Mjamaica huyo alitumia sekundi 19.78 na kumaliza mbele ya Mcanada Andre de Grasse na Mfaransa Christophe Lemaitre.
Muingereza Adam Gemili alimaliza sambamba na Lemaitre
Bolt, 29, tayari hapo awali kwenye Michuano hii ya jijini Rio ameshashinda mbio za mita 100, na leo Ijumaa itakuwa ni fainali ambapo atakimbia mbio za mita 4x100 (400).
Bolt anatarajiwa kurudia rekodi ya mafanikio yake ya kushinda mbio za mita 100, 200 na 4x100 aliyoiweka mwaka 2008 jijini Beijing na 2012 jijini London.
Mjamaica huyo, ambaye mwezi February mwaka huu alisema angependa kustaafu mwaka 2017 baada ya Michuano ya Dunia (World Championships), ameshinda fainali zote za nane Olimpiki ambazo amewahi kushiriki.
0 comments:
Post a Comment