Tuesday, August 9, 2016

Katika hali yoyote ile mtu kupata mafanikio kila wakati hujisikia vibaya pale anapopita  kwenye changamoto kubwa ya kutopata ile raha aliyozoea kwa muda mrefu. Katika mchezo wa soka, kiu kubwa ya mashabiki wa timu ni mafanikio kwa timu yao. 
Haijalishi mafanikio hayo yanakuja kwa namna ipi, lakini ili mradi yanaonekana na mashabiki wanapata faraja.

Wakati msimu wa 2015-16 unakaribia kuanza, United walikuwa hawana hali kutokana na ubora hafifu wa kikosi chao. Matumaini yao ya kushiriki Ligi ya Mabingwa yaliisha siku mbili tu kabla ya ligi kumalizika, na kuwafanya kukosa nafasi ya kushiriki michuano hiyo kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu. Walitwa ubingwa wa FA ambao hata hivyo hakuwa na ladha yoyote kwa Mashetani Wekundu hao wa Old Trafford na kuamua kuchukua maamuzi ya kumfukuza aliyekuwa kocha wa timu hiyo Louis van Gaal.

Ulikuwa ni moja ya misimu mibovu kwao baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha. Van Gaal aliwafanya Man United kutoogopwa tena kutokana na aina ya staili yao ya uchezaji. Timu vigogo na ndogo zilijichuliwa pointi bila woga. Haikuwa tena timu ambayo ilikuwa na uwezo wa kulazmisha matokeoa pale inapohitaji kufanya hivyo. Walishindwa hata kulinda ushindi wao mara kadhaa walipokuwa wakiongoza.

Uthibitisho wa ujio wa Paul Pogba kunako Dimba la Old Trafford kwa dili lililogharimu kiasi cha zaidi ya paundi mil 100, kumeanza kujenga picha mpya ya namna gani United itakuwa timu ya kuogopwa. Kutoka kuwa timu isiyohofiwa kwenye miaka ya hivi karibuni mpaka kuwa tena United inayoogopwa kama Simba mwenye njaa awapo mwituni.

Mwanzo kabisa, lilikuwa suala la ujio wa Mourinho kama meneja wa timu hiyo,  na baadaye mambo yakazidi kuiva baada ya kuwaleta Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan bila kumsahau Eric Bailly. Usajili wa Pogba kwenda United ni ishara kubwa kwa Mashetani Wekundu hao kuweza kupata mchezaji wa kaliba kuwa namna hiyo, huku timu ikiwa haishiriki Ligi ya Mabingwa. Ikumbukwe kuwa imekuwa vigumu sana kwa vilabu visivyo na nafasi ya kushiriki Uefa Champions League kuweza kuwavutia mastaa wa kiwango cha juu, lakini United wameweza, jiulize kwanini!!

Hebu jiulize, hivi ni klabu ngapi ambazo zitakuwa zikishriki Europa zimeweza kufanya usajili wa namna hii wa kuwaleta watu kama Pogba, Zlatan Mkhitaryan ambao wote bado walikuwa na nafasi ya kushiriki Uefa msimu huu? Tena mtu kama Zlatan ambaye anapambana katika nyakati hizi za mwisho za maisha yake ya soka kupata kombe la Uefa, ambalo hajawahi kupata halafu aje acheze Europa?

Siri ya yote haya ni kwamba, United wameamua kuwekeza nguvu zao zote kuhakikisha wanarudi. Licha ya timu kutofanya vyema chini ya utawala wa Moyes na Van Gaal, United bado wameendelea kuwa timu yenye nguvu kubwa ya pesa. Ed Woodward na baodi yake wameamua kufanya kweli nna kutohofia chochote juu ya matumizi ya fedha wakiwa na nia moja tu kuifanya United kuwa na nguvu kama wakati wa Mzee Ferguson,

Wameshatumia pesa nyingi kwenye usajili wa Angel Di Maria na Radamel Falcao miaka miwili iliyopita. Lakini bado wakafeli.pengine walikosea kufanya hayo chini ya utawala wa Van Gaal, lakini kwa sasa watakuwa wamefanya maamuzi sahihi kumwaga noti hizo kwa Mourinho, kocha ambaye huwa hakosei anapotengewa dau la kusajili mchezaji wa aina yeyote anayempenda,

Mreno huyo mwenye majivuno, aliorodhesha maeneo manne yenye udhafi ambayo angependa yafanyiwe kazi. Upande wa beki wa kati tayari Muivory Coast Eric Bailly, safu ya kiungo mshambuliaji kamchukua Mkhitaryan, safu ya ushambuliaji akamleta Zlata ambaye kazi yake tunaifahamu vyema. N sasa anamalizia na Pogba ambaye anakuja kukamata eneo la kiungo wa kati na kuifanya Man United kuwa na kikosi kinachotisha. Pogba anatajwa kuja kuziba pengo la Paul Scholes ambalo kwa muda mrefu limekosa mtu sahihi wa kulitendea haki.

Ikumbukwe tu kwamba tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson, inawezekana huu ndio usajili wa kwanza kabisa kufanywa kwa malengo ya hali ya juu kulingania na mahitaji. United wana nguvu ya pesa, na mabosi wa timu hiyo wanaonekana ni watu wanaoumizwa na matokeo mabovu ya timu hiyo, bila kusahau washabiki wao ambao wamekosa amani kwa muda mrefu sasa.

Kitu muhimu sana kilichobaki kwa sasa ni kuona washabiki wa United kutembea kifua mbelea msimu huu, wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema. Kwa misimu kadhaa walikuwa wanyonge wasio na cha kujivunia kutokana na kikosi chao kukosa nguvu ya kupambania ubingwa. Msimu huu unaonekana kuwa ni wa faraja kubwa kwao.

Huu ni mwanzo tu, lakini itawachukua takriban miezi 12 kabla kuanza kuonesha nguvu yao kwa mara nyingine tena katika soka la Ulaya tangu mwishoni mwa mwezi Mei, lakini kwa kesi ya Ligi ya England, hakuna shaka kwamba, United tayari wameanza kuonesha ishara ya kurejea katika hali waliyokuwa wakiiota kwa miaka ya hivi karibuni. Tusubiri na tuone hali itakavyokuwa mpaka kufika mwisho wa msimu huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video