Leicester City wanawakaribisha Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya pili ya EPL utakaopigwa kwenye uwanja wa King Power majira ya saa 1:30 za usiku.
Mabingwa hawa watetezi watakuwa na beki wao Robert Huth baada ya kumaliza kuitumikia adhabu yake ya kukosa michezo mitatu.
Jeff Schlupp atakwepo licha ya kuhusishwa na mipango ya kuhamia West Brom.
Arsene Wenger tayari amesema kwamba anaweza kucheza 'pata pote' kwa kuwachezesha nyota wake Laurent Koscielny, Mesut Ozil na Olivier Giroud, ambao walichelewa kujiunga na timu hiyo pre-season kutokana na kuzitumikia timu zao za taifa kwenye Michuano ya Euro 2016.
Aaron Ramsey na Alex Iwobi wote watakuwa nje kwa wiki tatu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya misuli ya paja na nyama za paja mtawalia.
Kauli za makocha kuelekea mchezo wa leo.
Meneja wa Leicester Claudio Ranieri juu ya Riyad Mahrez: "Sasa tupo Champions League na tunahitaji kitu fulani cha ziada ili kuweza kushindana na timu vigogo. Sasa anajua vizuri kitu gani nahitaji kutokana makubwa ninayotaraji kufanya. Sio tu kwa Riyad bali kwa wachezaji wangu wote.
"Amesaini mkataba wa miaka minne, na mimi pia kwasababu nataka kujenga timu imara. Anataka kufanya kitu tofauti pia, vivyo hivyo kwa Jamie Vardy, Kasper Schmeichel, na kila mchezaji kwenye timu. Ni vizuri sana."
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger: "Tuna idadi kubwa ya wachezaji ambao wanataka kuja Arsenal wakiwemo baadhi ambao wamewahi kucheza na baadaye kuondoka hapa ambao ni takriban asilimia 99.5%. Kuwavutia wachezaji kuja hapa si jambo gumu.
"Najua mnashawishiwa kuamini kwamba mimi sipendi kutumia pesa nyingi kwenye usajili, lakini nawahakikishia kwamba tupo tayari kutumia pesa. Ila kitu ambacho sikubaliani nacho ni kuamini kuwa njia pekee ya mafanikio kwenye soka ni kununua wachezaji.
Kununua wachezaji wapya haitoshi ila kununua wachezaji wapya bora ndiyo kitu cha msingi, nadhani hii ndio misingi iliyojengwa kwenye klabu hii."
Rekodi za mechi walizokutana (Head-to-head)
- Ndani ya michezo 19 waliyokutana na Arsenal kwenye Premier League hawajashinda hata mchezo mmoja (wamefungwa 13, sare 6).
- Arsenal wameshindwa kufunga kwenye mchezo mmoja tu kati ya 27 ya ligi waliyokutana, walitoka suluhu January 2001.
Leicester City
- Leicester City ni timu ya kwanza kama mabingwa watetezi kupoteza mchezo wa ufunguzi tangu Arsenal walivyofanya hivyo mwaka 1989. Hakuna bingwa mtetezi yeyote ambaye alianza ligi kwa vipigo mfululizo tangu ilivyowatokea Aston Villa mwaka 1981.
- Msimu uliopita Leicester wamecheza michezo minne ya Premier League bila ya Robert Huth kuanza kwenye kikosi, na katika michezo yote hiyo hawakuweza kupata clean sheets.
- Endapo Claudio Ranieri atashinda mchezo huu, utakuwa ni ushindi wake wa 100 kwenye mashindano.
Arsenal
- Arsenal hawajawahi kupoteza michezo miwili mfululizo ya ufunguzi ya ligi tangu msimu wa 1992-93.
- Arsenal wameruhusu magoli manne kwenye uwanja wao wa nyumbani wikiendi iliyopita kwa mara ya kwanza tangu Mei 2009, na mara ya tatu kwenye historia ya timu hiyo.
- Kipigo kutoka kwa Liverpool kilihitimisha mfululizo wa mechi 10 bila kufungwa.
- Alexi Sanchez amefunga magoli manne kwenye michezo miwili iliyopita katika dimba la King Power.
0 comments:
Post a Comment