Wednesday, August 10, 2016

Gary Neville amefanikiwa kurejesha kibarua chake kunako kituo cha runinga cha Sky Sports ambapo sasa atakuwa akilipwa paundi 300,000 baada ya kuwa mapumzikoni kufuatia kutimuliwa na klabu ya Valencia aliyokuwa akiifundisha.

Inaelezwa kwamba Neville atakuwa anapata paundi mil 1.5million kwa mwaka kutokana kwa kuonekana walau mara 40 akifanya uchambuzi wa Ligi ya England ikiwa ni pamoja na kufanya kazi nyingine za ziada kwenye kituo hicho.

Kumekuwa na ongezeko la maslahi kwake kutokana na hapo awali kabla ya kuondoka kuwa akilipwa paundi mil 1.2 kwa mwaka.
Gary Neville atakuwa akilipwa paundi 300,000 kama mchambuzi wa soka wa Sky Sports.

Wakati wachambuzi wengine wakilipwa kila wanapoalikwa, Neville amefanikiwa kurejea na kupewa nafasi ya kudumu licha ya kuwa na changamoto kubwa ya kuthibitisha ubora wake kufuatia rekodi mbaya aliyopata akiwa na Valencia kama kocha mkuu na England kama kocha msaidizi kwenye Michuano ya Euro mwaka 2016 iliyomalizika hivi karibuni.
Safari hii hataruhusiwa kufanya kazi nyingine yoyote mbali na Sky Sports tofauti na Thierry Henry, ambaye analipwa pesa nyingi zaidi lakini akiruhusiwa kujihusisha na masuala mengine.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video