Mkutano mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa klabu ya Yanga Africans unafanyika asubuhi hii kuanzia majira ya saa tatu kamili katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.
Wakati wengi wakiamini huenda Agenda ya Mabadiliko ya Mfumo wa Uendeshaji kutoka wanachama wa kawaida kwenda Mfumo wa Kampuni inaweza kuibuka kama ilivyo kwa watani zao wa jadi, Simba SC, huko Jangwani mambo bado hayajawekwa wazi.
Mratibu wa Matawi na Mkuu wa kitengo cha Masoko wa Young Africans SC, Omary Kaya, jana aliongea na waandishi wa habari kwa niaba ya uongozi wa klabu na kutaja Agenda ambazo zitatumika kwenye mkutano mkuu wa wanachama leo ambazo ni:
1.Mwenendo wa timu kiujumla.
2.Mahusiano kati ya Young Africans na TFF
3.Katiba ya Young Africans SC
4.Mapato na Matumizi ya Klabu.
5.Shukrani kwa Wajumbe waliomaliza muda wao.
6.Kuishukuru Serikali kwa ushirikiano wanaonyesha kwenye mashindano tunayoshiriki.
7.Maendeleo ya klabu.
8.Mengineyo.
Labda suala la Mabadiliko linaweza kujadiliwa katika Agenda namba 7 ya Maendeleo ya klabu au namba 8-Mengineyo.
Wakati huu zipo taarifa zinazoeleza kwamba huenda Yanga wakaanza mchakato wa kuingia kwenye mfumo wa kampuni ambapo Hisa zitauzwa kwa wanachama, huku mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji akitajwa kuwa atafanya kama Mohamed Dewji 'MO' katika klabu ya Simba, ingawa ni kwa dau tofauti.
Wakati huo huo, kikosi cha Yanga, jioni ya leo uwanja wa Taifa, Dar es salaam kuanzia saa 10:00 kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar na Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu Tano (5,000/-) kwa Majukwaa yote
0 comments:
Post a Comment