1.MO kupewa 51%
2. Viongozi wa Simba kumuandikia MO barua.
*NITAELEZA KWA UFUPI*.
*1. MO KUPEWA 51%.*
Bila shaka huo ni mpango usio na umuhimu wowote licha ya MO kusema kuwa nia yake ni kuisaidia Simba.
Kama hiyo ndio nia yake Basi hata akiwa na 49% atakuwa katoa msaada mkubwa tu kwani msaada hauna kiwango.
Ila kwa wenye Kufikiri... Wataona wazi kuwa nia ya MO ni ya UTAWALA NA BIASHARA.
Anakusudia kujenga Wigo mpana wa Maamuzi na Iwapo Simba haitakuwa na Wanasheria wazuri na Wasionunulika basi Kuna Hatari siku Moja tukasikia Simba imebadili jina na Kuitwa Paka. (Ndio maana ya Mmiliki.. Ana Maamuzi ya Mwisho).
Kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla ya MO au Mtu yeyote kupewa Umiliki wa Taasisi ya Pamoja.
*DHAMIRA, DIRA, HADHI, HESHIMA, UTAMADUNI, MALI, MUDA, KIWANGO... HAYO YOTE NI MUHIMU KUZINGATIWA KATIKA MKATABA KWA MANUFAA YA WENGI.*
Makosa yoyote yatakayofanyika hapo yatasababisha Matatizo makubwa hadi kwa Amani ya Nchi. (Wenye Kufikiri Watanielewa).
*2.VIONGOZI WA SIMBA KUMUANDIKIA BARUA MO.*
Kwangu hiki ni Kichekesho cha Mwaka katika Weledi wa Kiuongozi.
MO alijitokeza kwenye Vyombo Vya Habari kutangaza nia yake... Hata mimi nikiamua naweza kufanya hivyo... Kwa nini baada ya nia hiyo asitoe tamko kuwa yuko mbioni kuuandikia barua uongozi wa Simba ili wazungumzie uwezekano huo wa yeye kununua hisa??
Kuna Maswali machache..
1.Nani mwenye haki ya Kutangaza Bei ya Hisa na Idadi ya Hisa zinazouzwa kati ya MO na Viongozi wa Simba kwa Niaba ya Wanachama??..
2.Kuna hakika gani kuwa MO ana nia hiyo bila kuuandikia uongozi wa Simba ili uwasilishe taarifa hiyo kwa wanachama??..
(Ina Maana kesho na Mimi nikiita Vyombo vya Habari kutangaza nia... Viongozi wa Simba wataniandiia kuniita??).
(Ina Maana kesho na Mimi nikiita Vyombo vya Habari kutangaza nia... Viongozi wa Simba wataniandiia kuniita??).
3.Je, utaratibu wa kununua hisa kwa Simba ni huo wa kutangaza nia au kuleta maombi rasmi kwa mujibu wa Taratibu zitakazowekwa?
4.Je, Ni MO peke yake Nchini au Duniani anayetaka kuwekeza Simba??
5.Kwanini Viongozi wa Simba wasitangaze uamuzi wa kuuza hisa ili kuleta ushindani??
6.Je, Kikao cha Serena hakiwezi kuwa cha aidha 'BIASHARA AU KUKOMOANA'??..
Umakini Unahitaji kabla ya Kukidhi Haja ya Mhemko.
Uchambuzi huu umeandikwa na Mchambuzi wa soka Chiki Mchoma... 0712 885 999.
0 comments:
Post a Comment