Beki wa Valencia Shkodran Mustafi na Arsenal wamefikia makubaliano binafsi kwaajili ya mchezaji huyo kujiunga na klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa ligi. Inaelezwa dili hilo litakamilika wikiendi hii.
Arsene Wenger anahitaji kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya mabeki wake Per Mertesacker na Gabriel Paulista kupata majeraha huku Laurent Koscielny akiwa bado hayupo tayari kutokana na kuchelewa kujiunga na wenzake kufuatia kupata mapumziko baada ya Michuano ya Euro.
Baada ya kutumia siku mbili kwaajili ya mazungumzo juu ya dili la mchezaji huyo, hatimaye wakala waa Mustafi amethibitisha kwamba dili sasa lipo mbioni kukamilika, huku Arsenal wakitakiwa kumalizana na klabu ikiwa ndiyo hatua ya mwisho.
"Shkodran na Arsenal wamefikia makubaliano, hatua iliyobaki ni Arsenal kumalizana na klabu yake ," Ali Bulut amesema ambaye ni wakala wa Mustafi.
0 comments:
Post a Comment