Friday, August 12, 2016

Azam FC leo inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Timu inayomilikiwa na Mamlaka ya Mapato ya Uganda, URA FC katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Awali mchezo huo ulitangazwa kuanza saa 10:00 jioni, lakini uongozi wa Wanalambalamba umebadili muda na sasa utaanza saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na kurushwa Live na AZAM SPORTS HD.
Afisa habari wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amesema sababu ya kubadilisha muda wa mechi ni kuwapa mashabiki nafasi nzuri ya kufika uwanjani.
"Tumeamua kubadili muda, sasa mechi dhidi ya URA itachezwa saa moja usiku. Leo ni siku ya kazi, kwahiyo tumesogeza muda ili watu wakitoka kazini wapate nafasi ya kuja". Amesema Jaffar, maarufu kama Mbunifu.
Viingilio katika mechi hiyo, VIP ni shilingi 3000/- na Mzunguko ni Buku tu! (1000/-).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video